1 Kings 10:14-19

14 aUzito wa dhahabu ambayo Sulemani alipokea kwa mwaka ulikuwa talanta 666,
Talanta 666 za dhahabu ni sawa na tani 25.
15 cmbali na mapato kutoka kwa wafanyabiashara na wachuuzi, na kutoka kwa wafalme wote wa Kiarabu na watawala wa nchi.

16Mfalme Sulemani akatengeneza ngao kubwa 200 kwa dhahabu iliyofuliwa; kila ngao ilikuwa na dhahabu yenye uzito wa shekeli 600
Shekeli 600 za dhahabu ni sawa na kilo 3.5.
17Akatengeneza pia ngao ndogo 300 za dhahabu iliyofuliwa, kila ngao ikiwa na uzito wa mane tatu
Mane tatu za dhahabu ni sawa na kilo 1.7.
za dhahabu. Mfalme akaziweka katika Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni.

18 fKisha mfalme akatengeneza kiti kikubwa cha kifalme kwa kutumia pembe za ndovu na kukifunika kwa dhahabu safi. 19 gKiti hicho kilikuwa na ngazi sita na egemeo la nyuma lilikuwa la mviringo kwa juu. Pande zote za kiti kulikuwa na mahali pa kuegemeza mikono, na simba wawili wakisimama kando ya hiyo mikono.
Copyright information for SwhKC